Perfect Builders

Perfect Builders Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Perfect Builders, P O BOX 35549, Dar es Salaam.

Licha ya kujitahidi kutafuta sana maisha lakini watu wengi hushindwa kujenga nyumba za ndoto zao kwa sababu hushindwa ku...
05/01/2024

Licha ya kujitahidi kutafuta sana maisha lakini watu wengi hushindwa kujenga nyumba za ndoto zao kwa sababu hushindwa kujua kwamba mradi wa kufanikisha kujenga nyumba ya ndoto yako unahitaji umakini mkubwa na kuna maeneo ya muhimu yanayopaswa kuzingatiwa lakini muhimu sana ni kupata mtu sahihi, mwenye uwezo na uzoefu wa kukuongoza kwa usahihi. Jambo hili hupelekea watu kupoteza pesa nyingi baada ya kukosea mwanzoni wakijaribu kurekebisha makosa yao nabado mara nyingi hushindwa kufanikisha kwa usahihi kile walicholenga kwa sababu kurekebisha makosa yote huhitaji gharama kubwa sana sawa na kuanza mradi upya kitu ambacho wengi wanakuwa hawana tena uwezo wa kumudu hilo....

Licha ya kujitahidi kutafuta sana maisha lakini watu wengi hushindwa kujenga nyumba za ndoto zao kwa sababu hushindwa kujua kwamba mradi wa kufanikisha kujenga nyumba ya ndoto yako unahitaji umakin…

Kwa sasa ni jambo ambalo liko wazi kabisa kwa kila mtu kwamba suala la wizi kwenye miradi ya ujenzi ni utamaduni uliokom...
31/12/2023

Kwa sasa ni jambo ambalo liko wazi kabisa kwa kila mtu kwamba suala la wizi kwenye miradi ya ujenzi ni utamaduni uliokomaa na kuota mizizi kabisa hasa kwa mafundi wa mitaani. Yaani kuiba imekuwa ni sehemu ya mbinu ambazo mafundi wameshazihalalisha kabisa kwao k**a njia ya kujipatia kipato na kwa wale wasiofanya hivyo ndio huonekana labda wana matatizo. Hii ni tabia na utamaduni wa hovyo sana lakini kwa bahati mbaya ni jambo ambalo ni vigumu sana kulikwepa ikiwa huna mikakati mikubwa na ambayo imezingatia kudhibiti kila njia na mbinu ambayo mafundi na wadau wengine huitumia katika namna ya kuiba katika maeneo ya ujenzi....

Kwa sasa ni jambo ambalo liko wazi kabisa kwa kila mtu kwamba suala la wizi kwenye miradi ya ujenzi ni utamaduni uliokomaa na kuota mizizi kabisa hasa kwa mafundi wa mitaani. Yaani kuiba imekuwa ni…

Moja kati ya sababu kubwa ya watu wengi kutopiga hatua kubwa kwenye maisha yao inatokana na watu kufanya mambo kwa mazoe...
16/12/2023

Moja kati ya sababu kubwa ya watu wengi kutopiga hatua kubwa kwenye maisha yao inatokana na watu kufanya mambo kwa mazoea na kufuata maneno na mazoea yaliyopo mtaani badala ya kukaa na kufikiri kwa utofauti. Mara nyingi kwenye maisha huwa tunakuja kugundua kwamba tulifanya makosa kwa kuchelewa sana wakati tukiwa tayari tumeshapoteza. Hili linachangiwa na ukweli kwamba binadamu huwa tunatumia zaidi hisia kwenye kuamua mambo badala ya kufikiri kwa kina juu ya madhara na faida ya kitu kwa muda mrefu....

Moja kati ya sababu kubwa ya watu wengi kutopiga hatua kubwa kwenye maisha yao inatokana na watu kufanya mambo kwa mazoea na kufuata maneno na mazoea yaliyopo mtaani badala ya kukaa na kufikiri kwa…

Watu wa zamani maarufu zaidi k**a “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ...
05/12/2023

Watu wa zamani maarufu zaidi k**a “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ukweli ni kwamba mara nyingi watu huwa hawaoni uzito wa jambo au changamoto kwa kuisikia tu kwa maneno k**a bado haijawatokea na ndio maana mambo yanapokwenda vizuri watu huchukulia kawaida na mara nyingi huwa hawashukuru wala kuonyesha kujali sana vile mambo yamekwenda vizuri....

Watu wa zamani maarufu zaidi k**a “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ukweli ni kwamba mara nyingi watu huwa hawaoni uzito wa jambo au changamoto k…

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma...
01/12/2023

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ikiwa mtu atafuata taratibu zilizowekwa ambazo zinahitaji mtu yeyote anayetaka kufanya mradi wa ujenzi kuzingatia mchakato mzima kuanzia kwenye zoezi la zabuni katika kupata washauri wote elekezi wa kitaalamu kwenye ujenzi kisha kupata mkandarasi baada ya zoezi la kukamilika kwa hatua za awali eneo la ushauri wa kitaalamu yaani michoro basi mtu huyo ana nafasi kubwa sana ya kukwepa changamoto hizi....

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ikiwa mtu atafuata tarati…

Katika makala zilizopita nimeeleza sana kuhusu changamoto za ujenzi ambapo changamoto mbili kuu zimekuwa ni uaminifu na ...
30/11/2023

Katika makala zilizopita nimeeleza sana kuhusu changamoto za ujenzi ambapo changamoto mbili kuu zimekuwa ni uaminifu na ubora. Watu wengi ambao bado hawajawahi kufanya ujenzi kwenye maisha yao wanaweza wasielewe kwa uzito unaostahili kuhusu changamoto hizi sugu sana ambazo zinaumiza sana watu kila siku. Watu ambao wameshapitia maumizi ya kuibiwa au kuharibiwa kazi au vyote viwili ndio wanafahamu kwa usahihi ni kiasi gani hizi ni changamoto kubwa sana....

Katika makala zilizopita nimeeleza sana kuhusu changamoto za ujenzi ambapo changamoto mbili kuu zimekuwa ni uaminifu na ubora. Watu wengi ambao bado hawajawahi kufanya ujenzi kwenye maisha yao wana…

Kwa watu ambao ambao wameshafanya ujenzi mara kwa mara wengi jambo hili limekuwa likiwashangaza kidogo, yaani sifa kuu w...
25/11/2023

Kwa watu ambao ambao wameshafanya ujenzi mara kwa mara wengi jambo hili limekuwa likiwashangaza kidogo, yaani sifa kuu waliyonayo mafundi wengi kwenye ujenzi ni kufanya wizi au udanganyifu kwa kila nafasi wanayopata. Hili limekuwa likiwashangaza wengi lakini ndio uhalisia, yaani kila nafasi inayopatikana ya kufanya wizi na udanganyifu basi huwa inatumiwa vizuri bila mtu kujali chochote. Kuna siku nilikuwa nimeenda kwenye eneo la mteja wetu mmoja kupima kabla ya kuanza kazi ya kuchora ramani husika tukawa tunajadili juu ya ujenzi wa mradi wake huo....

Kwa watu ambao ambao wameshafanya ujenzi mara kwa mara wengi jambo hili limekuwa likiwashangaza kidogo, yaani sifa kuu waliyonayo mafundi wengi kwenye ujenzi ni kufanya wizi au udanganyifu kwa kila…

24/11/2023

Katika nchi ambayo bado maeneo mengi hakuna mifumo imara sana ya udhibiti na katika jamii ambayo imeharibika kimaadili hasa katika yale maadili ya msingi k**a hizi nchi maskini za kiafrika basi moja kwa moja unategemea kwamba tabia k**a wizi kwenye eneo la ujenzi itakuwa ni kubwa. Ukweli ni kwamba wizi kwenye ujenzi ni k**a utamaduni wa mafundi, tabia hii imezagaa sana japo haizungumzwi kwa ukubwa na uzito inayoleta lakini madhara yake ni makubwa sana, yanaumiza sana watu na yanarudisha sana nyuma maendeleo ya watu....

Katika hii dunia thamani ya vitu hupimwa kwa namna nyingi na ubora wa huduma pia ni moja ya thamani ya vitu ambavyo hupi...
15/11/2023

Katika hii dunia thamani ya vitu hupimwa kwa namna nyingi na ubora wa huduma pia ni moja ya thamani ya vitu ambavyo hupimwa kwa namna nyingi. Huduma za ukandarasi na ujenzi mbali na kupimwa kwa uwezo, vifaa na wataalamu pia hupimwa kwa unafuu na uharaka wa ukamilishaji wa mradi wa ujenzi kwenye eneo la muda. Wote tunajua kwamba muda wenyewe ni fedha na hivyo kuutumia vibaya ni kupoteza fedha....

Katika hii dunia thamani ya vitu hupimwa kwa namna nyingi na ubora wa huduma pia ni moja ya thamani ya vitu ambavyo hupimwa kwa namna nyingi. Huduma za ukandarasi na ujenzi mbali na kupimwa kwa uwe…

Wote tunajua kwamba binadamu wengi kwa asili tuna asili ya ubinafsi na kuangalia kile tunachokipata katika jambo lolote ...
12/11/2023

Wote tunajua kwamba binadamu wengi kwa asili tuna asili ya ubinafsi na kuangalia kile tunachokipata katika jambo lolote tunaloamua kulifanya. Hakuna tatizo kwenye tabia hii ya asili kwa sababu kwanza ndio iliyosaidia dunia kufika hapa ilipofikia. Tatizo linakuja pale ambapo asili hii inakuwa ndio kitu pekee kinachomsukuma mtu bila kujali wala kujishughulisha na ubora wa ile huduma au bidhaa unayotoa kwa sababu hujali kabisa kuhusu watu na utu wao....

Wote tunajua kwamba binadamu wengi kwa asili tuna asili ya ubinafsi na kuangalia kile tunachokipata katika jambo lolote tunaloamua kulifanya. Hakuna tatizo kwenye tabia hii ya asili kwa sababu kwan…

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. H...
08/11/2023

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. Hii ni kwa sababu mvuto au uzuri wa jengo hausababishwi na kitu kimoja pakee bali ni muunganiko wa vitu vingi vilivyofanyika kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni fulani maalum ndio hupelekea jengo kuwa na mvuto huo wa aina yake. Muunganiko huu huhusisha kila kitu kinachooneka kwenye jengo kuanzia chini mpaka juu na kwa kuzingatia sifa zote za vipengele husika vya jengo....

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. Hii ni kwa sababu mvuto au uzuri wa jengo hausababishwi na kitu kimoja pakee b…

Baada ya msingi wa jengo kuchimbwa na kisha kumwagwa kwa zege ya chini kabisa kwenye msingi(blinding concrete) na kujeng...
05/11/2023

Baada ya msingi wa jengo kuchimbwa na kisha kumwagwa kwa zege ya chini kabisa kwenye msingi(blinding concrete) na kujengwa kwa tofali za kwenye msingi kinachofuata huwa ni kurudishia udongo kwenye msingi kujaza yale maeneo ulipoondolewa na hakujajengwa. Zoezi la kurudishia udongo kwa lugha ya kitaalamu huitwa, “backfilling”. Lakini hata hivyo mara nyingi hutokea kwamba udongo wa eneo husika ambao ndio umechimbwa chini kwa ajili ya kupisha ujenzi wa msingi hutokea kwamba huwa haufai kurudishia kwa sababu ni udongo hatari sana kwa usalama wa nyumba au jengo linalokwenda kujengwa eneo hilo....

Baada ya msingi wa jengo kuchimbwa na kisha kumwagwa kwa zege ya chini kabisa kwenye msingi(blinding concrete) na kujengwa kwa tofali za kwenye msingi kinachofuata huwa ni kurudishia udongo kwenye …

Address

P O BOX 35549
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Perfect Builders posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share