msanifu majengo wa mtaa

msanifu majengo wa mtaa Architect/ Digital content creator/ General life updates đź’Ş

Historia ya Jumatano ya Majivu(kwa wakatoliki — Ash Wednesday kwa Kiingereza) ni hii:‎‎Muundo wa Historia‎Asili yake ili...
19/02/2026

Historia ya Jumatano ya Majivu(kwa wakatoliki — Ash Wednesday kwa Kiingereza) ni hii:
‎
‎Muundo wa Historia
‎Asili yake ilikuwa na ishara ya toba na majivu, tangu zamani za Agano la Kale, ambapo watu waliweka majivu juu ya miili yao kuonyesha toba, huzuni, na unyenyekevu mbele za Mungu (Kitabu cha Biblia Katika Agano la Kale kuna mfano wa matumizi ya majivu k**a ishara ya toba (k**a Daniel 9:3; Yonah 3:5–6).
‎Katika zama za Kanisa la Kikristo, imani ya kutumia majivu kuonyesha toba ilianza kuchukuliwa k**a ishara ya kuanza msimu wa Kwaresima kipindi cha siku 40 za kufunga na toba kabla ya Pasaka kulingana na makalaya Encyclopedia Britannica.
‎Majivu kutumika rasmi k**a taratibu za liturujia ya Jumapili ya Majivu (Ash Wednesday) ilianza kutumika katika Kanisa Katoliki kabla ya karne ya 8, na jadi hii ilienea zaidi ulimwenguni kulingana na makala ya Friars.
‎
‎Mnamo mwaka 1091, Papa Urbano II aliamuru kanuni hii ya kupokea majivu iweze kutumika rasmi kwa Kanisa lote la Kirumi na kuitwa “Feria Quarta Cinerum”(Jumatano ya Majivu) k**a mwanzo wa Kwaresima katika makala ya ukrasa wa Catholic Education / Catholic Online.
‎
‎
‎
‎
‎

Tanzania Yaomba Ushirikiano wa China Kujenga Uwanja wa Kisasa Arusha kwa AFCON‎‎Serikali ya Tanzania imeiomba rasmi Seri...
10/02/2026

Tanzania Yaomba Ushirikiano wa China Kujenga Uwanja wa Kisasa Arusha kwa AFCON
‎
‎Serikali ya Tanzania imeiomba rasmi Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kushirikiana nayo katika ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofanyika kwa pamoja kati ya Tanzania, Kenya na Uganda.
‎
‎Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali na kunukuliwa na Gazeti la Mwananchi, ombi hilo limewasilishwa katika mazungumzo ya kidiplomasia kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, likilenga kuimarisha miundombinu ya michezo na kukuza uchumi wa kanda ya Kaskazini mwa Tanzania.
‎
‎Uwanja huo unaoendelea kujengwa Arusha unalenga kukidhi viwango vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), sambamba na kuongeza idadi ya viwanja vya kimataifa nchini. Serikali imesisitiza kuwa Arusha ni mji wa kimkakati kutokana na nafasi yake ya kijiografia, utalii na miundombinu ya usafiri.
‎
‎China, ambayo imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya michezo barani Afrika, imetajwa kuwa na uzoefu mkubwa unaoweza kusaidia kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa wakati.
‎
‎Kwa mujibu wa Mwananchi, ujenzi wa uwanja huo hautasaidia tu maandalizi ya AFCON bali pia utafungua fursa za ajira kwa vijana, kukuza michezo, kuongeza mapato ya utalii na kuifanya Arusha kuwa kitovu cha matukio ya kimataifa ya michezo.
‎
‎Serikali imeeleza kuwa mazungumzo bado yanaendelea, huku ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania inakuwa tayari kikamilifu kuandaa mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

‎

Usajili wa Karim Benzema, mshambuliaji maarufu wa Ufaransa na mshindi wa Ballon d’Or, amefanikiwa kujiunga na klabu ya A...
04/02/2026

Usajili wa Karim Benzema, mshambuliaji maarufu wa Ufaransa na mshindi wa Ballon d’Or, amefanikiwa kujiunga na klabu ya Al-Hilalya Saudi Pro League kwa mkataba wa miezi 18 (hadi Juni 2027)
‎
‎Uhamisho huu ulifanyika kwa sababu
‎ Al-Ittihad waliamua kumwachilia FREE baada ya Benzema kukataa mkataba wa upya ambao alikuwa ukimfanya apate pesa kidogo kuliko anavyostahili kulinganga na ukrasa mkubwa wa Flashscore.
‎ Hivyo, Benzema hakuhitaji ada ya usajili kwa Al-Hilal — ni free transfer kulingana na ukurasa The National umesema hivyo.
‎
‎Kiasi atakacholipwa Benzema,Ripoti za jana zilisema Benzema atakuwa akipata mkataba mzito sana nchini Saudi hadi takriban €1.1 m sawa na bilioni 3.36 za kitanzania kwa wiki chini ya mkataba wake kulingana ukurasa mkubwa wa SPORTbible.

‎

SIMULIZI LILILOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU SHABIKI NA SADIO MANÉKuna simulizi lililosambaa sana mitandaoni kuhusu shabiki m...
02/02/2026

SIMULIZI LILILOSAMBAA MITANDAONI KUHUSU SHABIKI NA SADIO MANÉ

Kuna simulizi lililosambaa sana mitandaoni kuhusu shabiki mmoja wa Sadio Mané, nyota wa soka kutoka Senegal. Inadaiwa kuwa dada huyo, anayesemekana kuitwa Aminata Diallo, anatoka Dakar, Senegal, aliwahi kujaribu kumkumbatis Sadio Mané lakini hakupata nafasi hiyo kwa sababu ya mavazi yake.

Kwa mujibu wa simulizi hilo, Sadio Mané alieleza wazi kuwa maisha yake yanaongozwa na misingi ya dini ya Kiislamu, na heshima, maadili pamoja na mavazi ya staha ni sehemu muhimu sana ya imani yake. Kwa sababu hiyo, inasemekana kuwa hakuwa tayari kuingia kwenye mahusiano ambayo hayazingatii misingi hiyo.

Baada ya muda, simulizi linaeleza kuwa yule dada aliamua kujibadilisha, si kwa ajili ya kumfurahisha mtu, bali kwa kuelewa na kuheshimu maadili ya dini na utamaduni. Alianza kuvaa kwa staha, kujiweka kwa heshima, na kuonyesha mwenendo unaoendana na maadili ya Kiislamu.

Ndipo simulizi linaendelea kudai kuwa mabadiliko hayo yalivutia heshima ya Sadio Mané na kupata nafasi ya kuonana nae na kumkumbatis tena, ambaye mara nyingi amekuwa akisisitiza kuwa uzuri wa kweli kwa mwanamke uko kwenye tabia, maadili na heshima, si mwonekano wa nje pekee.

Hadithi hii imekuwa ikitumiwa na wengi k**a funzo: kwamba si kila kukataliwa ni chuki, bali wakati mwingine ni msimamo wa kimaadili. Pia inaonyesha kuwa mabadiliko ya kweli huanzia ndani ya mtu mwenyewe.

01/02/2026

Address

Dar/es/salaam
Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when msanifu majengo wa mtaa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share