Ndege Construction

Ndege Construction Pata Makazi Bora Kwa Ramani Yako Kwa Gharama Nafuu

Kwa nini UKUTA hupukutika?________Inasababishwa na unyevu utokao chini ya ardhi, k**a eneo halina chumvi madhara yake ya...
23/11/2024

Kwa nini UKUTA hupukutika?
________

Inasababishwa na unyevu utokao chini ya ardhi, k**a eneo halina chumvi madhara yake yanaenda taratibu, na k**a eneo lina asili ya chumvi basi madhara yake yataenda kwa haraka zaidi.

Nini kifanyike?
Ni kujenga inavyotakiwa.

Kujenga inavyotakiwa ndo nini?
Ni kujenga kwa kufuata taratibu na kanuni za ujenzi.

Ndo maana yake nini?
Katika suala la kuzuia ukuta usipukutike, kanuni ya ujenzi inatwambia tutumie DPC na DPM inavyotakiwa.

DPC ndo nini?
~Hiki ni kifupi cha maneno ya kiingereza ikimaanisha Damp Proof Course, kwa kiswahili inamaanisha ni tabaka linalowekwa kwa ajili ya kuzuia unyevu usipite.

DPM ndo nini?
~Hiki ni kifupi cha maneno ya kiingereza ikimaanisha Damp Proof Membrane, kwa kiswahili ni tabaka linalowekwa kuzuia unyevu usipite

Kuna tofauti gani kati ya DPC na DPM ?
~Tofauti ipo,

DPC huwekwa juu ya msingi wa mawe au juu ya msingi wa tofali au juu ya mkanda wa zege uliwekwa juu ya msingi au huwekwa juu ya zege la jamvi kabla kuweka mstari(kozi) wa kwanza wa tofali, ili tofali ya kwanza ikae juu ya mota ya simenti iliwekwa juu ya DPC. Iwekwe kwa kuzidi upande wa ndani na nje ili hata plasta inakuja kulala juu ya hiyo DPC, pia sehemu za kuunga hakikisha unaipishanisha kiasi kisichopungua 20 sentimita. Hii hufanyika ili kuzuia maji yatokayo ardhini kupanda na ukuta.

Material inayoweza kutumika k**a DPC ni nyingi lakini zinazopatika kwa matumizi ni zile zilizo katika mfumo wa rola ya lami, kuna nzito, na kuna zile za laini na kuna saizi ya kati. Hufungwa kwa urefu wa wastani wa mita 10 na upana wa mita 1.

DPM huwekwa juu ya mchanga uliowekwa juu ya jiwe(hardcore) au huwekwa juu ya mchanga baada ya kunyunyuzia dawa ya mchwa. Ikishawekwa vizuri kwa kupishanisha inavyotakiwa unaweza kumimina zege la jamvi juu ya hiyo DPM.

Lengo la kuweka DPM ni nini?
~Kuzuia unyevu kuja katika sakafu.

Kwani unyevu kuja kwenye sakafu kuna shida gani?
~Shida ipo!

Usipoweka hii sakafu itakuwa ya baridi sana kipindi cha masika, inaweza kusababisha vitu kupata uvundo na kupelekea kuoza, inasababisha nyumba isifae kwa matumizi ya binadamu kwa sababu itakuwa ya baridi sana wakati wa masika na pia hata wakati mwingine k**a utakuwa umejenga sehemu ambayo inakuwa na unyevu muda wote wa mwaka.

Hii iko kwenye mfumo wa rola ya karatasi nylon nyeusi nzito ambayo hupatikana katika duka la vifaa vya ujenzi tu.

Kujenga inavyotakiwa inawezekana | 0754 565 136

Jengo linapoanguka jiulize maswali haya:______1) Je matumizi yaliyokusudiwa bado yako vilevile? Hakuna kilichoongezwa au...
19/11/2024

Jengo linapoanguka jiulize maswali haya:
______

1) Je matumizi yaliyokusudiwa bado yako vilevile? Hakuna kilichoongezwa au kubadilishwa?
2) Mhandisi alishirikishwa kabla na wakati wa ujenzi?
3) Kablasha la mahesabu ya mhandisi katika hilo jengo lipo?
4) Saizi ya nguzo ilikuwa inatosha?
5) Saizi ya beam ilikuwa inatosha?
6) Saizi ya slab ilikuwa inatosha?
7) Nondo zilizotumika ni aina gani ? Za saizi gani ?Zilipimwa maabara? Zilipangwaje?
8) Saruji aina gani ilitumika? Ilipimwa kila ilipoletwa saiti? Ni Uwiano gani wa zege ulitumika?
9) Msingi ulikuwa kimo gani kwenda ardhini? Nguzo za msingi zilikuwa na saizi gani? Udongo ulipimwa?
10)Kokoto aina gani zilitumika? Zilipimwa maabara?

10/09/2024
Je hakuna ubaya nondo kupakwa rangi?
16/08/2024

Je hakuna ubaya nondo kupakwa rangi?

Yaweza kuwa ni nini?
15/08/2024

Yaweza kuwa ni nini?

Unajua nini kuhusu Prestress Concrete?..Hii ni pale ambapo waya za aina yake hutumika ndani ya zege kwa lengo la kuipa z...
08/08/2024

Unajua nini kuhusu Prestress Concrete?..
Hii ni pale ambapo waya za aina yake hutumika ndani ya zege kwa lengo la kuipa zege uimara wa kuweza kusapoti uzito unaotegemewa kubebwa na hiyo zege.

Mara nyingi hii hutumika kwenye zege linalosapotiwa upande mmoja(cantilever) au kwenye madaraja na hata kwenye mataluma ya zege.

DPC ni kifupi cha maneno ya kiingereza(Damp Proof Course) ,ni materials ambayo inatumika katika ujenzi wa nyumba kuzuia ...
23/03/2024

DPC ni kifupi cha maneno ya kiingereza(Damp Proof Course) ,
ni materials ambayo inatumika katika ujenzi wa nyumba kuzuia unyevu usipande kutoka ardhini kuja kuharibu ukuta.

Usipotumia madhara na hasara ni kubwa kuliko bei ya kununulia hiyo matilio.

Mfano wa ukuta ambao nyumba ilijengwa bila kutumia DPC angalia picha ya pili.

Hivi ndivyo beam inavyofanya kazi,K**a una mzigo mkubwa wa kubeba unaongeza kimo cha beam
22/12/2023

Hivi ndivyo beam inavyofanya kazi,
K**a una mzigo mkubwa wa kubeba unaongeza kimo cha beam

Chukua na hii
22/12/2023

Chukua na hii

Katika picha kuna vifaa kadhaa, taja ulichowahi kutumia
19/12/2023

Katika picha kuna vifaa kadhaa, taja ulichowahi kutumia

Je ni wakati gani tunaweka linta, na ni wakati gani tunaweka ringibeam ?Linta = Ni kipande cha zege ambacho huwekwa juu ...
19/12/2023

Je ni wakati gani tunaweka linta, na ni wakati gani tunaweka ringibeam ?

Linta = Ni kipande cha zege ambacho huwekwa juu ya uwazi wa mlango au juu ya uwazi wa dirisha

Ringibeam = ni mkanda wa zege unaowekwa juu ya uwazi wa milango na madirisha kuzunguka nyumba nzima

Address

Dar Es Salaam
00255

Telephone

0754 565 136

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ndege Construction posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share