FAABI Electrical Service Provider Ltd.

FAABI Electrical Service Provider Ltd. Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from FAABI Electrical Service Provider Ltd., Electrician, Sinza E. Near TP Ground, Dar es Salaam.

Tunahusika na ufungaji wa waya (Wiring) majumbani, Ushauri kuhusu matumizi sahihi ya Umeme, Kukagua mifumo ya Umeme majumbani na viwandani, kuuza na kusambaza vifaa vya Umeme pamoja na mifumo ya Ulinzi na usalama Majumbani pamoja na viwandani

26/05/2026

MOJA YA SEHEMU YA KUWA KIONGOZI NI KUONESHA KIVITENDO HUO UONGOZI ULIVYO ILI WALE UNAOWAOONGOZA WAFANYE K**A VILE UNAVYOHITAJI WAFANYE.

MAMBO YA KUZINGATIA ZAIDI WAKATI WA UWEKAJI WA NJIA ZA MIFUMO YA UMEME, CCTV CAMERA NA FIRE ALARM SYSTEM kwenye SLAB kab...
06/05/2026

MAMBO YA KUZINGATIA ZAIDI WAKATI WA UWEKAJI WA NJIA ZA MIFUMO YA UMEME, CCTV CAMERA NA FIRE ALARM SYSTEM kwenye SLAB kabla ya UMWAGAJJ WA ZEGE:

(1)Kujua kuisoma na kuitafsiri ramani kujua ina mahitaji yapi na yapi kwenye mifumo ya Umeme.

(2)Kuweka njia za kutosha Kwa Kila Circuit na ikitokea njia ya upande mmoj imeziba basi unatumia njia nyingine iliyo jirani yake wakati wa kuvuta waya

(3)Kuzilinda na kuhakikisha njia za Circuit yako zinaeleweka.

(5) Hakikisha round boxes zako zinakamata vyema na Marin bodi bila kunyanyuka, hakikisha round boxes zako umeziweka makatatasi au mifuko ya cement vyema kuzuia zege kuingia.

(6) Hakikisha kila chumba kinakuwa na njia zaidi ya moja kwenda kuchukua Supply power kutoka kwenye Main switch.

(7) Hakikisha kwenye main conduit utakazopeleka zisiwe chini ya 25mm hii itakusaidia kuwa na conduit chache na uhakika wa kuvuta Circuit zaidi ya Tatu kwenye njia moja wakati wa Wiring.

(8) Punguza safari ndefu ya Conduits pipes kati ya points A kwenda Point B hasa wakati unatengeneza POWER CIRCUIT

(9) Hakikisha Kazi yako unaifanya Kwa weledi na muda wa kutosha na si kufanya Kazi Kwa shinikizo na kupewa muda mchache na msimamizi wa Jengo au Mkandarasi wa jengo hii itakupa nafasi ya kufanya Kazi sahihi na kwenye makosa ni rahisi kurekebisha sababu muda unao wa kutosha.

(10) Siku ya kumwaga zege kuwa karibu zaidi na Kazi yako wewe mwenyewe au Kwa mtu ambaye unamuamini ili kuhakikisha hakuna Conduits pipes itakayopata madhara baada ya zoezi kukamilika.

(11)KWEPA MATERIALS FEKI HASA CONDUITS PIPES SABABU ZIKIZIBA AU KUPASUKA WAKATI WA ZEGE UTAONEKANA WEWE FUNDI NDIYO MZEMBE NA SI CLIENT ALIYEKULETEA
MATERIALS FEKI.

(12)AGIZA MATERIALS ZA KUTOSHA NA SI KUMPA CLIENT AU MKANDARASI HESABU NDOGO YA MATERIALS ALAFU BAADAE UOMBE TENA MATERIALS.

Andiko hili limeandikwa Nami:
Ibrahim Makbel Jr.
+255
0777077755
0787577755

This is a 63A adjustable over-voltage and under-voltage protective device for single-phase electrical systems.Functional...
01/05/2026

This is a 63A adjustable over-voltage and under-voltage protective device for single-phase electrical systems.Functionality: It safeguards electrical equipment by automatically disconnecting power if voltage exceeds 300V, drops below 140V, or if current exceeds the set limit (1-63A).Display and Control: The unit features a dual LED display to independently show real-time voltage and current, with buttons to set protection thresholds.

Siyo GOOGLE PICTURE NI kazi halisia kabisa ikifanywa nasi FAABI Electrical Service Provider Ltd
19/04/2026

Siyo GOOGLE PICTURE NI kazi halisia kabisa ikifanywa nasi FAABI Electrical Service Provider Ltd

SHINE WITH US FAABI Electrical Service Provider Ltd. 0777077755078757775507675777550717577755Kibaha, Coast Region, Tanza...
07/04/2026

SHINE WITH US FAABI Electrical Service Provider Ltd.

0777077755
0787577755
0767577755
0717577755

Kibaha, Coast Region, Tanzania 🇹🇿

10/03/2026

THE INSTALLATION OF ELECTRICAL SYSTEMS ON THE SECOND FLOOR HAS FINALLY BEEN COMPLETED ✔️

0777077755
0787577755
0767577755
0717577755
KIBAHA COAST REGION, TANZANIA 🇹🇿

10/03/2026

Dodoma Nzuguni Site:
Tayari sisi hapa FAABI Electrical Service Provider Ltd. tumekamilisha hatua ya Circuit design, uvutaji wa Waya (Wiring) pamoja na maandalizi ya Control Room kwa ajili ya ugawaji wa Umeme kwenye Nyumba za Client wetu huyu ambapo Mita zote za Umeme, Generator au Backup power ya Solar system itaanzia kwenye control Room inayoandaliwa kisasa zaidi nasi

FAABI Electrical Service Provider Ltd
0777077755
0787577755
0767577755
0717577755
Kibaha Coast Region, Tanzania 🇹🇿

12/12/2025

KABLA YA KULALAMIKA MATUMIZI MAKUBWA YA UMEME KWENYE JENGO LAKO HAKIKISHA FUNDI WAKO ALIFANYA VIPIMO SAHIHI KABLA NA BAADA YA MATUMIZI YAKO YA UMEME.

SOMA KWENYE ANDIKO LANGU HILI HAPA UPATE CHA KUJIFUNZA.

"Kwanza kabisa Mafundi wengi hawajui kufanya VIPIMO vya Umeme baada ya kukamilisha mifumo ya Umeme (Wiring)
Pili mafundi wengi hufanya kazi za mifumo ya Umeme kwa mazoea bila kufanya vipimo vya Umeme.

Vipimo hivi Basic na muhimu baada ya kumaliza kusuka mifumo ya Umeme.

(1l) CONTINUITY TEST
Kipimo hiki kitahakikisha Circuit yako imekamilika na umeifanya Wiring yako kwa usahihi na kifaa kinachoweza kupima kipimio hiki ni Multimeter na utaweka kipimo chako kwenye upande wa Ohm's

(2)VERIFICATION OF POLARITY Kipimo hiki kitahakikisha kuwa hakuna muingiliano wa L waya kwenda E au N waya na kipimo hiki kitakuhakikishia L waya ipo sehemu sahihi kuanzia kwenye Main switch kwenda kwenye Circuit husika hivyo hivyo kwa upande wa N na E. Na kipimio utakachotumia hapa ni Multimeter na utaweka kwenye Range ya Ohm's

(3)INSULATION TEST kipimo hiki ambacho mafundi wengi HUKIKWEPA ni kipimo muhimu mno ambacho kinahakikisha ubora wa INSULATION ya waya ulizotumia, Usalama wa kazi yako baada ya kukamilisha Wiring. Na kipimo hiki sasa kikisoma Ohm's kubwa ya Insulation yako basi kaa ukijua Wiring yako ni mbovu na haina ubora na Insulation ya waya zako ina Leakage na kipimio kinachotumika hapa ni MEGA.

(4)EARTH TEST Kipimo kingine ambacho mafundi wengi hukikwepa na ni muhimu ni HIKI HAPA. Kipimo hiki kitahakiki ubora wa EARTH Ground yako na kuhakikisha hakuna current zitakazopotea au mtumiaji kupata madhara na kipimo hiki kinapaswa kufanywa kabla ya Client hajaanza matumizi ya Umeme kwenye jengo lake. Na kipimio kinachotumika hapa ni EARTH GROUND TESTER.

(5)LOAD TEST kipimo hiki nacho mafundi wengi hawajawai hata kukitumia. Baada ya kukamilisha vipimo vyako vyote kuanzia namba 1 hadi 4 kipimo cha mwisho sasa ni hiki ambacho baada ya Client wako kuhamia na kuanza matumizi yake kwa ujumla inapaswa kumpimia kujua ndani ya lisaa limoja anatumia KILO WATTS ngapi? Na kipimo hiki ndiyo kinakuwa finally ya vipimo vyote na hapa utatumia kipimo cha CLAMP ON METER AU MULTIMETER na utaweka Range yako kwenye upande wa Current kisha utamalizia kwenye upande wa VOLTAGE.

HAKIKISHA VIFAA VYOTE VINAVYOTUMIA UMEME KWA WAKATI HUO VINAFANYA KAZI ILI KUPATA TOTAL CURRENT SAHIHI KISHA UTAZIDISHA KWA VOLTAGE ILI KUPATA WATTS KISHA UTAGAWA KWA 1,000 ILI KUPATA TOTAL KILO WATTS

Ibrahim Makbel Jr.
0777077755
Asanteni

Muonekano bora wa jengo lako huletwa na Design bora ya Taa pamoja na mifumo bora ya Umeme. Fanya yote ila usije ukakosea...
10/12/2025

Muonekano bora wa jengo lako huletwa na Design bora ya Taa pamoja na mifumo bora ya Umeme.
Fanya yote ila usije ukakosea kwenye suala zima la mifumo ya Umeme na wa kukupa Muonekano bora wa jengo lako kwa upande wa Umeme si wengine ila ni sisi hapa:
FAABI Electrical Service Provider Ltd

Wasiliana nasi sasa:
0777077755
0787577755
0767577755
0717577755

Address

Sinza E. Near TP Ground
Dar Es Salaam
45563

Opening Hours

Monday 09:00 - 19:00
Tuesday 09:00 - 19:00
Wednesday 09:00 - 19:00
Thursday 09:00 - 19:00
Friday 09:00 - 19:00
Saturday 09:00 - 19:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FAABI Electrical Service Provider Ltd. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to FAABI Electrical Service Provider Ltd.:

Share

Category