03/09/2026
Miaka kumi na saba. Kiwango kimoja cha ubora.
Jana, ALAF ilitunukiwa katika Tuzo za 19 za Raisi za Wazalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA), zilizoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), ambapo kwa fahari kubwa tulishika Nafasi ya 1 katika kipingele cha Vyuma na Bidhaa za Vyuma kwa mwaka wa 17 mfululizo
Ushindi huu unaakisi dhamira yetu ya kuendelea kutoa bidhaa zenye ubora wa kimataifa, kuendeleza ubunifu na kuchangia ukuaji wa sekta ya viwanda nchini Tanzania.
Kwa CTI, timu yetu nzuri, na kila mteja anayeendelea kujenga nasi, tunawashukuru kwa imani na ushirikiano wenu unaoendelea. Pamoja, tutaendelea kujenga sekta imara ya viwanda, jamii imara na Tanzania imara zaidi.