30/05/2016
Habari za sasa hivi,
leo naomba tujuzane ufugaji mseto wa samaki,mifugo na kilimo (mbogamboga).
INTEGRATED AQUACULTURE AND AGRICULTURE (IAA)
Ufugaji huu umeanza muda mrefu lakini wafugaji wengi huwa hawatumii. baada ya kuchimba bwawa la samaki na kukamilika jenga banda la kuku,bata juu yabwawa la samaki kwenye kona moja ya bwawa ambako kuna kina kifupi na eneo unapolishia samaki. kwa mifugo aina ya ng'ombe, mbuzi na wengine unaweza tengeneza mfereji mwembamba kutoka kwenye banda la mifugo kwenda kwenda kwenye bwawa la samaki. samadikutoka kwenye mifugo hutumika k**a chanzo cha mbolea ambayoinarutubishamaji kwenye bwawa lasamaki. Hii husaidia kuzalisha viluiluividogo vya jamii ya mimea (phytoplanktons) na wanyama (zooplanktons) ambavyo hutumika k**a chakula kwasamaki wafugwao. idadi ya wanyama watakao hitajika ilikurutubisha maji kwenye bwawa la samaki inategemea na ukubwa wa bwawa lako.Mfano:- bwawa lenye ukubwa wa mita 6*10M unaweza kuweka kuku/bata 10, ng'ombe mmoja, mbuzi/kondoo 3. ufgugaji huu husaidia kuhakikisha chakula ndani ya bwawa la samaki kuwa na chakula wakati wote. pia chakula cha aina hii kinakiasi kingi cha protini about (60%). Eneo karibu na bwawa la samaki linafaa kwa kilimo cha mbogamboga ambazo baadayamuda mfupi hukomaa na kuvuna ndani ya muda mfupi, mfano (bilinganya, hoho, mchicha, spinachi,bamia na mengineo). Maji kutoka kwenye bwawa la samaki hutumika kumwagilizia mbogamboga na kumbuk**aji hayo yana virtubisho vingi kutoka kwenye mbolea za wanyama ambavyo huhitajika na mimea kwa ukuaji.
ufugaji huu una faida mbalimbali
1. samaki
utapata mazao kutoka kwenye bwawa la samaki kwa kupata samaki
2. mbogamboga
hii husaidia kuongea mapato kwa mfugai na unaweza ukalima mchanganyiko wa mbogamboga nyingi kutokana na ukubwa wa eneo ululonalo.
3.malisho ya mifugo
mabaki mbalimbali kutoka kwenye mabaki ya mbogamboga hutumika k**a chakula kwa wanyama
4. ulinzi
kadri shughuli za uzalishaji zinavyozidi kuwa nyingi maeneo kuzunguka bwawa husaidia kulinda samaki wasishambuliwe na ndege pamoja naviumbe wengine ikiwemo binadamu ambao wanaweza kuwadhuru samakii kwa njia moja au nyingine.
5. matumizi mazuri ya rasilimali aridhi na maji
mseto wa shughuli hizi katika eneo moja husaidia kupunguza matumizii ya aridhi. Eneo dogo la aridhi linaweza kuzalisha mazao mbalimbali na mengi.
6. kupunguza uchafuzi wa mazingira
kwa ufugaji wa samaki wa aina hii husaidia maji kutoka kwenye bwwa la samaki kutoyaachia kwenda sehemu mbalimbali na kuchafua mazingira kutokana na vituvilivyomo ndani yake bali hutumika kumwagilizia mazao.
NOTE: inashauriwa kuweka mpira kwa ajili ya kufyonza maji kutoka kwenye bwawa la samaki ili kupunguza kuchafua maji ya bwawa. pia unaweza kutumia maji ya ndani ya bwawa la samaki kwa kumwagilizia wakati wowote muda wa ufugaji. kiasi cha maji ambayo yatapunguzwa ndani ya bwawa kwa ajili ya kumwagilizia mbogamboga inatakiwa kijazwe mara moja ili isijedhuru ukuajii wa samaki ndani ya bwawa la samaki.
leo nilipenda kushirikishana nanyi juu ya huu ufugaji mseto wa samaki, mifugo na kilimo. mapendekezo,nyongeza au maswali yanakalibishwa na sote kwa ujumla tutashiriki katika kujibu.
Naomba kuwasilisha
RealAquaculture