22/07/2025
๐๐ก๐. ๐๐๐ญ๐๐ฆ๐๐ข ๐๐ค๐๐๐ข๐๐ก๐ข ๐๐๐ฌ๐ฆ๐ข ๐๐ง๐๐จ ๐ฅ๐ ๐๐ซ๐๐๐ข ๐ค๐ฐ๐ ๐๐๐ ๐๐ฅ๐จ๐๐๐ฅ ๐๐ฎ๐ฅ๐ญ๐ข ๐๐จ๐ง๐ญ๐ซ๐๐๐ญ๐จ๐ซ๐ฌ ๐๐ก๐ข๐ง๐ฒ๐๐ง๐ ๐
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, ameongoza hafla fupi ya kukabidhi eneo la mradi kwa mkandarasi AMJ Global Multi Contractors Company Limited, kwa ajili ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa na barabara yenye urefu wa kilomita 6.5 katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Katambi aliipongeza kampuni hiyo kwa kupewa jukumu la utekelezaji wa mradi huo muhimu na kusisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi wa maeneo ya jirani kwenye ajira zitakazopatikana wakati wa ujenzi.
โ๐๐ช ๐ฎ๐ข๐ต๐ข๐ณ๐ข๐ซ๐ช๐ฐ ๐บ๐ฆ๐ต๐ถ ๐ฌ๐ถ๐ธ๐ข ๐๐๐ ๐๐ญ๐ฐ๐ฃ๐ข๐ญ ๐ธ๐ข๐ต๐ข๐ฉ๐ข๐ฌ๐ช๐ฌ๐ช๐ด๐ฉ๐ข ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ฏ๐ค๐ฉ๐ช ๐ธ๐ข ๐๐ฉ๐ช๐ฏ๐บ๐ข๐ฏ๐จ๐ข, ๐ฉ๐ข๐ด๐ข ๐ธ๐ข ๐ฎ๐ข๐ฆ๐ฏ๐ฆ๐ฐ ๐บ๐ข๐ฏ๐ข๐บ๐ฐ๐ป๐ถ๐ฏ๐จ๐ถ๐ฌ๐ข ๐ฎ๐ณ๐ข๐ฅ๐ช ๐ฉ๐ถ๐ถ, ๐ธ๐ข๐ฏ๐ข๐ฑ๐ฆ๐ธ๐ข ๐ง๐ถ๐ณ๐ด๐ข ๐ป๐ข ๐ข๐ซ๐ช๐ณ๐ข ๐ช๐ญ๐ช ๐ธ๐ข๐ด๐ฉ๐ช๐ณ๐ช๐ฌ๐ช ๐ฎ๐ฐ๐ซ๐ข ๐ฌ๐ธ๐ข ๐ฎo๐ซ๐ข ๐ฌ๐ข๐ต๐ช๐ฌ๐ข ๐ฎ๐ข๐ฆ๐ฏ๐ฅ๐ฆ๐ญ๐ฆ๐ฐ ๐บ๐ข ๐ฎ๐ซ๐ช ๐ธ๐ข๐ฐ,โ alisema Mhe. Katambi.
Mradi huu unalenga kuboresha huduma za usafiri, kuongeza ufanisi wa miundombinu ya usafirishaji, pamoja na kuchochea uchumi wa maeneo ya mjini Shinyanga. Pia unatarajiwa kutoa ajira kwa vijana na wakazi wa mji huo, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya serikali ya awamu ya sita ya kuimarisha maisha ya wananchi kupitia miradi ya kimkakati.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, viongozi wa dini na wananchi, ikiwa ni ishara ya mshikamano wa pamoja katika kuleta maendeleo.