Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit

Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit VIFARANGA NA VIATAMIZI

Tunauza vifaranga, na pia tunatengeneza Mashine za kuangulia vifaranga
Mashine tunazotengeneza za kuangulia vifaranga zina ufanisi mkubwa sana

SHAMBANI KWETU LEOWale wanaohitaji incubator ya mtindo huu.Hii ni incubator ambayo ufanisi wake ni mpaka 90%Hii ni ya mt...
04/01/2026

SHAMBANI KWETU LEO
Wale wanaohitaji incubator ya mtindo huu.
Hii ni incubator ambayo ufanisi wake ni mpaka 90%
Hii ni ya mteja na imeelekea Kagera.
Karibuni sana.
0756282827

SHAMBANI KWETU LEOMAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKEKila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha n...
25/12/2025

SHAMBANI KWETU LEO
MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE
Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu

NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.

GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe k**a chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na k**a matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukak**aa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya k**a vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic k**a Otc 20%.

MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za uso, kichwa na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.

FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.

FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.

MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.

K**a utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo k**a utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi

SHAMBANI KWETU LEOKwa wale wanaofuga vifaranga wengi kwa pamoja, hii ni heater inayotumia oil chafu kwenye chumba cha vi...
21/10/2025

SHAMBANI KWETU LEO
Kwa wale wanaofuga vifaranga wengi kwa pamoja, hii ni heater inayotumia oil chafu kwenye chumba cha vifaranga. Haina moshi wala hewa yoyote chafu. Hii inatosha vifaranga 500 hadi 3000
KARIBUNI 0756282827

28/09/2025

SHAMBANI KWETU LEO
Matumizi ya jiko la oil chafu ili kupunguza gharama za kuzalisha joto kwa vifaranga

22/09/2025

SHAMBANI KWETU LEO

05/08/2025

SHAMBANI KWETU LEO:

20/07/2025

Shambani kwetu leo

22/06/2025

SHAMBANI KWETU LEO
TANGAZO:
Kwa wale wanaohitaji huduma ya kutotolesha mayai, huduma inapatikana muda wowote na kwa mayai idadi yoyote.
Mnakaribishwa wote.
Tupo Tagamenda. Kwa wale wanakuwa hawana muda wa kufika Tagamenda fanya mawasiliano ili upokelewe mayai mjini.
Karibuni sana
0756282827, 0655903809 na 0753903809

02/06/2025

Shambani kwetu leo:
TANGAZO. TANGAZO. TANGAZO
Kwa wale wote wenye mayai yao ya kuku na ya bata na ya kanga na yana mbegu, na pia yapo ndani ya muda; hayajazidi umri wa siku 10, yaleteni tuwatotoleshee kwa bei ya kawaida kabisa.
Idada yoyote ya mayai tunapokea; kuanzia yai moja hadi mayai elfu kumi.
KARIBUNI WOTE 0756282827

Kwa wale wanaohitaji kutengezewa mashine kubwa na zenye ufanisi mkubwa wa kutotoa mayai ya kuku, bata, kanga, nk. karibu...
16/05/2025

Kwa wale wanaohitaji kutengezewa mashine kubwa na zenye ufanisi mkubwa wa kutotoa mayai ya kuku, bata, kanga, nk. karibuni sana. Mashine zetu ni kuanzia mayai machache kiasi cha mayai 88 hadi 10,000.
Mashine zetu ni imara sana na zina ufanisi mkubwa.
Kwa mawasiliano 0756282827, 0753903809, 0762361388, 0655903809.

SHAMBANI KWETU LEO:Construction of a 10,000 egg incubator cm hatcher.This incubator is for our client in Morogoro
16/05/2025

SHAMBANI KWETU LEO:
Construction of a 10,000 egg incubator cm hatcher.
This incubator is for our client in Morogoro

Shambani kwetu leo:JINSI YA KUHIFADHI MAYAI YA KUTOTOLESHA. 1.  Sehemu ya yai iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.2....
21/04/2025

Shambani kwetu leo:
JINSI YA KUHIFADHI MAYAI YA KUTOTOLESHA.

1. Sehemu ya yai iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.

2. Hifadhi sehemu yenye kupitisha hewa ya kutosha na isiyokuwa na joto.

3. Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku yalipotagwa.

SIFA YA MAYAI YA KUATAMIWA.
Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumika nyumbani kwa chakula. Sifa za mayai mazuri ya kuatamiwa ni k**a ifuatavyo...

1. Yawe masafi na wala yasisafishwe au kufutwa na kitambaa chenye maji k**a ni machafu.

2. Yasiwe na nyufa.

3. Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo.

4. Yawe na ukubwa wa wastani kulingana na
umbile au aina ya kuku.

5. Yasiwe ya mviringo k**a mpira pia yasiwe na ncha kali.

6. Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka siku yalipotagwa.

7. Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

Kwa ushauri zaidi 0756282827

Address

TAGAMENDA, IRINGA
Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit:

Share