Meridian Capitals ltd.

Meridian Capitals ltd. Meridian Capitals for better life

19/05/2024

DPC ni nini?
DPC ni kifupi cha maneno ya kiingereza, Damp Proof Course, ikimaanisha kozi inayojengwa(kuwekwa) ili kuzuia unyevu.

Ntaijuaje?
Hii material huuzwa katika baadhi ya maduka ya vifaa vya ujenzi. Iko kwenye umbo la rola nyeusi nzito, ukiikata inakatika kirahisi sana, ina upana wa mita moja na urefu wa takribani mita 10, hizi ndizo ziko sokoni kwa wingi lakini zipo pia kwa vipimo tofauti.

Kwa nini iuzwe katika maduka baadhi?
Inauzwa katika maduka baadhi kwa sababu wengi hawaijui hii material hivyo ni vigumu kuiweka kwenye orodha ya bidhaa unayoenda kununua.

Kwa nini lazima tuitumie?
Ni lazima kuitumia ili kuhakikisha ukuta wa nyumba unadumu kwa kuzuia unyevu utokao ardhini kupanda na ukuta.

Mbona tumetumia lakini mvua ikinyesha maji yanapanda?
~K**a ulitumia DPC lakini kipindi cha mvua kuta zinalowa, basi ujue ilitumika ndivyo sivyo.

MATUMIZI SAHIHI.
~K**a ukuta ni wa kulaza tofali hakikisha unakata upana ambao itatokeza huku na huku ili ukipiga plasta iegemee kwenye hiyo material lasivyo unvyevu utapanda na plasta.
~K**a ukuta ni wa kusimama halikadhalika hakikisha DPC inatokeza huku na huku kiasi cha kutosha. K**a una tofali nzuri na fundi wazuri wa kuweza kunyosha ukuta ndani na nje vizuri basi DPC inaweza kutokeza inchi moja huku na huku lasivyo itokeza zaidi ya hiyo inchi moja.
~Pia kwenye ovalap, hakikisha zinapishana vya kutosha.

Muhimu:
Hata k**a wakati wa kujenga huoni dalili ya maji toka ardhini, bora kuweka DPC kwa sababu huwezi kujua baada ya miaka 10 au 20 nini kitatokea eneo hilo.

Utajuaje nyumba haikuwekwa DPC ?
~Utaona chini ya dirisha hadi kwenye msingi nyumba mbichi, tofali zimeliwa, plasta imeliwa, malumalu inalia sauti ya ngoma, rangi imevimba n.k

K**a nimeshajenga bila kutumia DPC nifanyeje?
~Tafuta fundi aiweke, ingawaje kuna usumbufu na gharama lakini ni bora kuliko kuacha nyumba ioze.

Madhara yatokanyo na kutoweka DPC?
~Nyumba kutodumu
~Nyumba kuwa ya baridi sana
~Gharama za matengenezo ya mara kwa mara.

17/05/2024
17/05/2024
Zanzibar door
15/05/2024

Zanzibar door

Maisha ni nyumba
14/05/2024

Maisha ni nyumba

Address

SHUNU
Kahama
MECA

Telephone

+255767150077

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Meridian Capitals ltd. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Meridian Capitals ltd.:

Share

Category