13/05/2022
KWANINI UWEKEZE KWENYE MITIBIASHARA?
Ni dhahili fursa zilizopo kwenye uwekezaji katika sekta ya misitu na msukumo endelevu wa ukuaji wake, unawahakikishia wakulima wadogo na wakubwa uboreshaji wa uchumi na mazingira.
Mambo MATANO muhimu kuzingatiwa katika uwekezaji katika sekta ya misitu;
1. Mahitaji ya Miti Kuongezeka.
Kufikia mwaka wa 2030, mahitaji ya mbao yataongezeka kwa mara mbili ya sasa na sababu ya kupungua kwa misitu ya asili, kuboreshwa kwa bidhaa za misitu na kuongezeka kwa idadi ya watu.
2. Bei ya Miti kuongezeka zaidi.
Kuadimika kwa mazao ya misitu sokoni kunapanua fulsa ya biashara na thamani ya uwekezaji katika sekta ya misitu nchini. Mti huongezeka thamani kadri unavyokua zaidi ya mfumuko wa bei. Kwa mujibu wa mwekezaji Jeremy Grantham, bei mbao katika karne iliyopita (~ 1905-2005) thamani ya mazao ya miti imeongezeka kwa takriban 3% zaidi ya mfumuko wa bei.
3. Miti inaweza kurudisha faida zaidi kuliko hasara.
Biashara ya miti inauwezekano wa kulipa zaidi ya kupata hasara (Risk/Return Trade off). Hii inamaanisha biashara hii ina ambatana na hatari kubwa ya kuanguka lakini ikiwa na uwezekano mzuri wa faida kubwa katika kuzingatia maamuzi ya uwekezaji. Hata hivyo misitu ina inaweza kubaki na thamani wakati mwingine hata k**a ikiharibiwa na moto au majanga ya asili pia ardhi yake kupandwa miti mingine kwa faida zaidi.
4. Miti ina uwiano chini katika madaraja mengine ya mali.
Thamani ya miti shambani inaongezeka siku hadi siku na kuweka tofauti ya soko la uchumi mkubwa kuliko madaraja mengine ya mali/uwekezaji. Pia soko la miti sio rahisi kuathirika kirahisi ukilinganisha na madaraja mengine ya mali, k**a vile bidha za maghalani, mali fungani na mali isiyohamishika.
5. Uwekezaji katika ardhi na thamani yake.
Ingawa Ardhi muhimu ya kupanda miti inaweza kukodishwa, lakini wawekezaji wengi wa miti wanapenda kununua ardhi k**a fulsa nyingine ya ewekezaji. Ukuaji wa thamani ya ardhi ni moja ya faida muhimu kwa mwekezaji wa miti kwani upatikanaji wake unapungua na mahitaji yake yanakua kwa sababu ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo ya kibiashara.
Tanzania kuna fulsa nzuri ya uwekezaji katika maeneo mengi yanayostawisha mazao mengi ikiwemo miti ya aina mbalimbali.
Karibu sana Smart Agroforestry & Gen Supp Co Ltd upate ushauri wa kitaalamu na usimamizi uliotukuka kwenye biashara yako.