Ujenzi on Point

Ujenzi on Point Pata Huduma ya Ramani na ushauri kuhusu ujenzi

Ramani ya nyumba ya kisasa kubwa na nzuri kwa familia (Family house) yenye vitu muhimu.Ramani ina...~Sitting room (Sebul...
21/04/2024

Ramani ya nyumba ya kisasa kubwa na nzuri kwa familia (Family house) yenye vitu muhimu.
Ramani ina...
~Sitting room (Sebule)
~Vyumba vitatu vyote vina ukubwa wa kutosha kimoja master kikiwa na Dressing Room yake, kingine Self na cha mwisho ni single (Single Bedroom)
~Public toilet (choo cha kushea)
~Jiko na Dining ( sehemu ya kulia chakula)
~baraza ya mbele na nyuma ( Front & Rear Verrander) pamoja na Stoo
Ramani ina ukubwa wa mita 11.6 urefu kwa mita 13 upana

MAHITAJI:
Tofali 2000 za Block (ZA BOMA)
Tofali 1000 za Block (ZA MSINGI)
Bati pisi 80(ZA FUTI KUMI UREFU NA UPANA FUTI 3)

Kupata Plan na Ramani hii pamoja na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/ WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza Link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Miliki nyumba yako kwa kuanza ujenzi na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana.Hii inafaa sana kwa wanaoanza maisha, Ram...
20/04/2024

Miliki nyumba yako kwa kuanza ujenzi na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana.Hii inafaa sana kwa wanaoanza maisha, Ramani ina vitu vifuatavyo:-
~vyumba viwili vya kulala vyote vya kawaida
~sebule
~jiko
~public toilet na Bafu la kushea
~Baraza Moja { Entrance veranda}
~Ukubwa wa Ramani ni mita 7.5 urefu kwa mita 7.9 upana.
~Mahitaji: Tofali 1400 {za block kuanzia msingi mpaka boma}, Bati 38 { za urefu futi 10 na upana futi 3}. Kupata Ramani hii na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Jenga kwa Ramani kwa sababu nyumba ni Ramani.Jipatie Ramani hii ya vyumba vitatu, chumba kimoja masta, vyumba vingine vi...
13/04/2024

Jenga kwa Ramani kwa sababu nyumba ni Ramani.Jipatie Ramani hii ya vyumba vitatu, chumba kimoja masta, vyumba vingine viwili ni vya kawaida, pia ina;
~Sebule
~dining{chumba cha kulia chakula}
~Jiko
~Choo cha kushea na Bafu
~Baraza ya mbele na ya jikoni { Entrance & Kitchen Verandah}

~Ukubwa wa Ramani ni mita 11 urefu kwa mita 12.8 upana
~Mahitaji: Tofali 3000 { Tofali 1000 za msingi na Tofali 2000 za Boma} Bati pisi 70 { Bati za futi 10 urefu na upana futi 3}
~Kupata Ramani hii pamoja na nyengine kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

KAZI YA LINTA KATIKA JENGOLinta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika ku...
13/04/2024

KAZI YA LINTA KATIKA JENGO

Linta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika kuta za jengo ili kubeba mzigo juu yake.

maegemeo; ni kiungo kinachowekwa juu ya uwazi wa madirisha, milango, mageti n.k ili kuweza kubeba mzigo juu yake bila kunepa. Kiungo hiki ni muhimu kwani uwazi au kifaa kitakachojazwa katika uwazi huo kinakuwa hakina uwezo wa kutosha kubeba mzigo juu yake. Kazi ya linta ni sawa na kazi za mihimili (beam) na tao (arch) katika jengo, ijapokuwa linta hujengwa kiurahisi na kikawaida zaidi; haihitaji utaalamu sana. Linta hutumika pale ambapo mzigo unaobebwa sio mkubwa na pia urefu wa uwazi sio mkubwa; pale ambapo uwazi na mzigo ni mkubwa basi lazima utaalamu zaidi utumike na pia itumike mihimili au tao.

Kawaida Linta hubebwa juu ya tofali za jengo au mara nyingine juu ya nguzo za jengo; basi ni muhimu kuhakikisha kuwa ncha zake zinaingia na kufungwa vizuri katika kuta zinazobeba linta hiyo ili kuhakikisha linta ipo imara na kuta haziharibiki.

Kazi za linta

Kubeba mzigo juu ya uwazi katika kuta

Hii ni kazi kubwa ambayo mara nyingi hutumika kufanya. Pale inapotokea juu ya dirisha au mlango unapaswa kujenga tofali nyingine au kuweka kitu chochote chenye uzito na fremu ya mlango haina uwezo wa kubeba mzigo huo, basi linta hutumika kubeba mzigo huo kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha uimara na ubora. Mara nyingi urefu wa linta katika majumba yetu huishia mita 3; pale umbali unapozidi 2m au mzigo kuwa mkubwa basi lazima hatua zaidi za kitaalamu zipate kufuatwa ili kuhakikisha hakuna kunepa wala nyufa katika linta yako.

Pale ambapo mzigo utakaobebwa ni mkubwa (tanki la maji, sakafu ya zege n.k) basi hatua za kitaalamu zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uimara na usalama wa jengo lako.

Kulishikilia na kulifunga jengo kiuimara

Linta pia hufanya kazi ya kulifunga jengo kwa pamoja ili liwe imara na lisitetereke kwa kuyumba, upepo, tetemeko n.k. Jengo linapokuwa limefungwa kwa pamoja na linta basi hufanya kazi kwa pamoja na kusaidia upande ule ambao ni dhaifu au umelemewa na mzigo uweze kustahimili. Bila linta, jengo linaweza kupunguza kutengemaa na uthabiti.

Kikawaida kuta za jengo zinapokuwa ndefu zaidi basi zinapunguza uimara wake; Lakini pale tunapozifunga kuta hizi kwa linta basi tunaziongezea uimara na uwezo wa kubeba mzigo.

Kwa nyumba zile za matofali ya kupachika (interlocking blocks), linta ni muhimu sana katika kuhakikisha tofali zinakaa kwa pamoja bila kupanguka. Linta pia inasaidia kuzishika kona za nyumba katika uimara.

Kuzui nyufa katika jengo lako

Linta huzuia nyufa katika jengo lako zisivuke upande mwingine wa jengo. Linta hufanya kazi ya kuzikata nyufa hizo na kufanya upande mwingine wa jengo uwe salama. Uimara wa linta ndio unaofanya ufa usiendelee; pale ambapo nguvu ya ufa ikazidi uimara wa linta, basi upande mwingine nao utaupokea ule ufa. Ni muhimu kuhakikisha awali kuwa nyumba yako unaijenga vyema na kwa ubora ili nyufa zisitokee na k**a zikitokea basi linta itakusaidia tuu kuzui nyufa zisiendelee. Pale inapotokea udongo katika kiwanja chako una hali ya ufinyanzi, basi ni muhimu kuiimarisha nyumba yako tangu katika msingi kwa kufunga nondo na maboresho mengine ili kuweza kuifanya nyumba yako kuweza kuhimili nguvu ya udongo mfinyanzi.

Aina za linta (materials)

Linta yaweza kutengenezwa kwa material mbalimbali kutegemeana na teknolojia, utaalamu, Upatikanaji wa malighafi n.k.

Mawe bapa

Mawe yaliyobapa na katika umbo linalotakiwa huweza kutumika kufanya kazi ya linta katika jengo lako. Mawe yanaweza kuhitajika yachongwe vyema ili kuhakikisha umbo linalotakiwa linapatikana.

Utumiaji wa mawe ni mdogo sana na teknolojia hii imekuwa ikitumika miaka ya zamani zaidi haswa katika nchi za nje. Kikawaida ni vigumu kupata mawe yanayofaa kwa kazi hii hivyo huweza kuongeza gharama kwa kuongeza kuyachonga mawe yako.

Uimara wa mawe pia sio mkubwa kwa kazi k**a hii hasa pale tunapotaka kufanyia kazi katika uwazi mrefu kwani mawe hayana uwezo wa kubeba umbali mrefu.

Miti na mbao

Miti na mbao huweza kutumika k**a linta katika jengo lako k**a vitaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa; baadhi ya viwango ni kutooza/kuharibika mapema, uwezo wa kubeba mzigo juu yake, kukidhi viwango vya moto n.k. Mbao na miti vimekuwa vikitumika maeneo mbalimbali tangu miaka ya zamani mpaka leo. Pale vinapotumika vizuri huweza kusaidia vyema kabisa katika jengo lako na kulifanya kuwa imara.

Kutokana na changamoto za gharama, uimara, kuoza, moto n.k matumizi yake yamepungua miaka ya sikuhizi katika majengo mbalimbali.

Tofali

Pale tofali zinapopangwa vizuri na kitaalamu basi huweza kutumika kubeba mzigo juu ya uwazi salama kabisa. Utaalamu unahitajika katika upangaji wa tofali hizi. Mara nyingi aina ya tofali zinazotumika ni zile za kuchoma; ubora na uimara wake unahitajika ili kuhakikisha uimara wa linta itakayojengwa. Linta za tofali hazina uwezo mkubwa wa kubeba mzigo wa uwazi mrefu.

Chuma

Bomba za chuma huweza kutumika kufanya kazi hii ya linta katika jengo lako katika ubora. Utaalamu unahitajika kuweza kupangilia vyema namna ya kutumika. Ni muhimu kuweza kuhakikisha usalama dhidi ya kutu na moto.

Zege

Hii ni aina ya linta ambayo watu wengi wamekuwa wakitumia zaidi katika ujenzi wao. Linta hii mara nyingi huwekwa nondo ndani yake ili kuifanya imara na kuweza kubeba mzigo mkubwa na kwa umbali zaidi. Aina hii ya linta pia inasaidia kufanya nayo kazi kwa urahisi na kwa usalama zaidi dhidi ya moto, kutu na kuoza. Ni muhimu kuweza kuzipanga na kuzifunga nondo vizuri na pia kutumia zege iliyo katika kiwango kinachokubalika. Kwa nyumba zetu za kawaida, nondo za 12mm hulazwa mbili chini na mbili juu katika linta na kufungwa kwa ringi la 8mm na kufanya boksi la pembe nne kisha zege ya 1:2:4 humiminwa ili kutengeneza linta imara katika jengo lako. Linta ya zege inapofungwa katika kuta za jengo lako lote basi huweza kulifanya jengo lako litengemae kwa pamoja.



Mwisho, ni muhimu kuweza kujenga jengo lako katika ubora ili kuweza kuliongezea muda wa kudumu na kulifanya salama kwa kuishi. Ijapokuwa haya mambo yanahitaji utaalamu na yana gharama, ni muhimu kuweza kujenga na kuwekeza kwa faida. Linta katika jengo ni muhimu ili kuweza kulifanya jengo lako liwe imara na lenye kuvutia. Linta hulifanya jengo lako liwe imara na kulitengemaza kwa pamoja. Linta husaidia kuzuia nyufa kushambulia jengo lako. Ni muhimu kuweza kujenga jengo lako katika ubora kwajili ya usalama, uimara na uwekezaji.

Kwa mahitaji ya Ramani mbalimbali na ushauri kuhusu ujenzi Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

FAIDA ZA KUJENGA KWA MATOFALI YA KUCHOMA.Kuwa na nyumba ni malengo ya watanzania wengi.Iwe ni kwa kuanza maisha, kuanza ...
13/04/2024

FAIDA ZA KUJENGA KWA MATOFALI YA KUCHOMA.
Kuwa na nyumba ni malengo ya watanzania wengi.Iwe ni kwa kuanza maisha, kuanza familia na muenzi wako, au kuweza kuhama katika nyumba ya kupanga na kuwa na mahali utakapoita nyumbani. Nyumba ina umuhimu sana katika maisha ya wanadamu, na kwa wengi ni malengo yao kuu. Kujenga Nyumba bora iliyoimara inahitaji umakini sana katika kujenga na kupanga ujenzi wa nyumba yako ijayo. Hivyo ni muhimu sana kujua aina ya matofali bora katika ujenzi wa Nyumba ya ndoto zako. Hivyo leo nitakueleza faida za kujenga kwa matofali ya kuchoma.

Matofali ya kuchoma hayana gharama.

Ujenzi wa matofali ya kuchoma ni ujenzi wa bei nafuu na hauhitaji kipato kikubwa kujenga nyumba kwa matofali ya kuchoma, gharama hizo huwa ndogo kutokana na gharama ndogo ya matofali hayo ambayo huwa kati ya 150,200 300,400 hadi 600 katika bei ya soko ukilinganisha na gharama ya tofali ya cement ambayo gharama yake huenda hadi sh. 2000 kwa tofali moja katika bei ya soko.Matofali hayo hayahitaji watu wengi kwenye kujenga kwa kuwa hazina uzito mkubwa, ujenzi wake hauitaji watu wengi hivyo gharama ya kujenga hupungua.

Matofali ya kuchoma ni Imara.

Matofali ya kuchoma yanauwezo wa kudumu kwa miaka mingi kuliko matofali ya cement. Kwa kawaida matofali ya kuchoma yanauweza kudumu kwa miaka hadi mia tatu bila kuharibika wala kububujuka. Ulikilinganisha na matofali ya cement ambayo kudumu kwake ni kati ya miaka sitini hadi mia.Hivyo nyumba ya matofali ya kuchoma inauwezo wa kudumu kwa miaka mingi zaidi kuliko ya simenti.

Matofali ya kuchoma yana muonekano mzuri.

Matofali ya kuchoma huwa na muonekano mzuri wa kuvutia,Matofali ya kuchoma hayahitaji rangi wala finishing kufanya eneo la nyumba kupendeza, bali matofali haya yanauwezo mkubwa wakutunza mvuto wake k**a rangi na muundo, kwa miaka mingi bila kupoteza uhalisia na upya wake. Ndio maana eneo lijengwalo kwa matofali ya kuchoma linauwezo wakuonekana kwamba ni mpya ingawa inamiaka mingi.

Hivyo ni vyema kuchanganua na kufahamu ubora na umuhimu wa matofali ya kuchoma katika ujenzi wa nyumba bora na imara. Kwa kuwa wengi wanandoto za kuwa na nyumba iliyo na mvuto,hivyo matofali ya kuchoma ndio suluhisho hilo.

Kwa mahitaji ya Ramani mbalimbali na ushauri kuhusu ujenzi Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

UMUHIMU WA KUJENGA MSINGI IMARA KWENYE NYUMBA YAKO:Moja ya maamuzi mabovu kabisa ambayo hutakiwi kuyafanya linapokuja sw...
13/04/2024

UMUHIMU WA KUJENGA MSINGI IMARA KWENYE NYUMBA YAKO:

Moja ya maamuzi mabovu kabisa ambayo hutakiwi kuyafanya linapokuja swala la ujenzi wa nyumba yako ni kutokujenga msingi imara.

Leo rafiki yangu napenda kukushirikisha umuhimu wa kuwa na msingi imara. Utaweza kufahamu msingi imara ni upi na ni kwa namna gani utahakikisha unakuwa na msingi imara kabisa ili ujihakikishie ujenzi wa nyumba bora.

Msingi Imara kwa ufupi ni ule ambao unaweza kuhimili uzito wa jengo pamoja na nguvu kutoka nje k**a vile upepo, msukumo wa udongo, mitikisiko pamoja na nguvu nyingine za asili. Msingi huu unaweza ukajengwa kwa kutumia mawe, matofali ya block, Zege au malighafi nyingine ambazo zinakubalika kwenye ujenzi. Unapokuwa na msingi imara unajihakikishia usalama wako, mali zako na wote watakaoishi ndani ya nyumba yako na pia utaweza kujikinga kwa namna Fulani na majanga ya asili k**a vile matetemeko na mitikisiko ya ardhi.

Hatua Tatu Muhimu Ujenzi wa Msingi Imara:

~Namna ya kuhakikisha unajenga msingi imara
Ili kuweza kujenga msingi imara na utakaosaidia kuimarisha jengo lako zingatia mambo yafuatayo;
i. Fanya utafiti wa eneo lako hasa katika kutambua aina ya udongo
Hapa unaweza ukafanya hata utafiti wa macho tu na kwa kushirikiana na mtaalamu wako wa ujenzi ukaweza kufanya maamuzi ya msingi utakaohitajika. Wakati mwingine udongo wa juu ya ardhi unaweza ukawa tofauti na ule uliopo ndani ya ardhi baada ya kuchimba mita kadhaa na endapo utakutana na hali hii basi msingi wako itabidi ubadilike kulingana na aina ya udongo uliyokutana nayo. Cha kuzingatia hapa ni kuhakikisha msingi wako unakaa juu ya sehemu ngumu na imara ili kuepuka kutitia.

ii. Tambua k**a eneo lako lina maji maji au ni eneo kavu
Msingi unaojengwa sehemu zenye majimaji ni tofauti kabisa na msingi utakaojengwa sehemu kavu. Kwa eneo ambalo lina maji muda mrefu msingi wake utahitaji material (mali ghafi) zinazoweza kuhimili uwepo wa maji k**a vile zege. Ukijenga msingi wa matofali ya kawaida kwenye eneo hili unajiweka kwenye hatari kubwa sana

iii. Jua matumizi sahihi ya Jengo lako
Kwa kutambua matumizi sahihi ya jengo lako kunasaidia sana katika kutambua uzito sahihi utakaohitajika kubebwa na msingi wako. Msingi wa nyumba ya kuishi ni tofauti sana na msingi wa ghala hivyo usijenge nyumba ya kuishi halafu baada ya muda unaibadilisha na kuwa ghala utaleta matatizo kwenye msingi.

Ninachotaka kukukumbusha rafiki yangu leo ni kwamba msingi ndio sehemu ya kwanza muhimu kwenye jengo lako na kamwe hutakiwi kufanya makosa kwenye eneo hili.

Kitu kingine ambacho ningependa kusisitiza ni kwamba USIJENGE KWA MAZOEA. Epuka kabisa maneno ya mtaani eti mbona Fulani amejenga hivi au vile na wewe ukayapokea yalivyo. Itakapotokea tatizo itakuwa ni wewe na wale watakaokuwa wanaishi ndani ya nyumba hiyo.

Jenga msingi imara uwe na nyumba bora maisha yako yote. Kwa mahitaji ya Ramani mbalimbali na ushauri kuhusu ujenzi Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Pata Huduma ya Ramani na ushauri kuhusu ujenzi
13/04/2024

Pata Huduma ya Ramani na ushauri kuhusu ujenzi

Ramani ya nyumba ya kisasa ya gharama nafuu ( simple Design) yenye mahitaji muhimu, ina..                           ~Seb...
12/04/2024

Ramani ya nyumba ya kisasa ya gharama nafuu ( simple Design) yenye mahitaji muhimu, ina..
~Sebule
~dining
~vyumba vitatu vya kulala kimoja master
~jiko. ~stoo
~public toilet
~entrance veranda {Baraza ya mbele}
~kitchen veranda { Baraza ya nyuma}
RAMANI INA UKUBWA WA MITA 8.9 UPANA KWA MITA 12.3 UREFU
MAHITAJI:
TOFALI 2800 (za msingi 800, za nyumba 2000)
BATI PISI 65 (za futi 10 urefu na upana futi 3) Kupata Ramani hii na nyingine kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza Link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Ramani ya nyumba ndogo yenye mahitaji muhimu, ina..~Sebule~dining~vyumba viwili vya kulala kimoja master~jiko~public toi...
12/04/2024

Ramani ya nyumba ndogo yenye mahitaji muhimu, ina..
~Sebule
~dining
~vyumba viwili vya kulala kimoja master
~jiko
~public toilet
~entrance veranda {Baraza ya mbele}
~kitchen veranda { Baraza ya nyuma}
RAMANI INA UKUBWA WA MITA 8.8 UREFU KWA MITA 10 UPANA
MAHITAJI:
TOFALI 1800 ZA BLOCK (Kuanzia msingi mpaka Boma)
BATI PISI 45 (za futi 10 urefu na upana futi 3) Kupata Ramani hii na nyingine kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza Link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Timiza ndoto yako na malengo ya kumiliki nyumba nakuwa na kwako kwa kujenga nyumba na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu ...
12/04/2024

Timiza ndoto yako na malengo ya kumiliki nyumba nakuwa na kwako kwa kujenga nyumba na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana simple Design ( Haina mambo mengi) pia wenye viwanja vidogo hii itawafaa sana
Ramani ina ukubwa wa mita 9.3 urefu kwa mita 9.1 upana. Ramani ina vitu vifuatavyo ndani:-
-Sitting room (sebule)
- kitchen ( jiko)
- Vyumba viwili vyote ni master ( 2 Master bedrooms)
-Baraza mbili ( Entrance and Kitchen veranda)

~Mahitaji
-Bati pisi 45 za futi 10 urefu na upana futi 3
-Tofali za Block 1800 ( kuanzia msingi mpaka boma)

Kupata Ramani hii na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇 https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Nyumba ni Ramani, Anza ujenzi wako na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana ( Simple Design) Haina mambo mengi.Ramani i...
12/04/2024

Nyumba ni Ramani, Anza ujenzi wako na Ramani hii ndogo ya gharama nafuu sana ( Simple Design) Haina mambo mengi.Ramani ina vitu vifuatavyo:-
~Vyumba vitatu vya kulala kimoja ni master
~choo cha public
~Jiko
~Sebule
~Baraza ya nyuma na mbele {Entrance & Kitchen verandah}
~Mahitaji:
Matofali 2000 ya block ya kuchoma ni 4000
Bati 60 za futi 10 urefu na upana futi 3

Ramani ina ukubwa wa mita 10.4 urefu na upana mita 10.3
Kupata Ramani hii na nyingine Kulingana na mahitaji yako Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp Au 0676056663 Call/SMS Au bonyeza link hapo chini 👇
https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1

Address

Moshi

Telephone

+255676056663

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ujenzi on Point posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ujenzi on Point:

Share