Forest Industries Training Institute - FITI

Forest Industries Training Institute - FITI We offer Technician certificate in Forest Industries Technology and various short courses including

Dirisha la Pili lipo wazi.
08/09/2026

Dirisha la Pili lipo wazi.

TAARIFA KWA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA FITI KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027.
28/08/2026

TAARIFA KWA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA FITI KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027.

Tunawatakia Maulid Njema
25/08/2026

Tunawatakia Maulid Njema

Watumishi na Wanafunzi wa Chuo Cha Viwanda vya Misitu Leo Tarehe 23 Agosti 2026 wameshiriki mbio za Hisani katika tukio ...
23/08/2026

Watumishi na Wanafunzi wa Chuo Cha Viwanda vya Misitu Leo Tarehe 23 Agosti 2026 wameshiriki mbio za Hisani katika tukio la TUKACHARU lililofanyika katika Msitu wa RAU Moshi Mjini.

MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO FITI.Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya M...
22/08/2026

MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO FITI.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Abdallah Mvungi, leo tarehe 22 Agosti 2026 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa pamoja na ile iliyokamilishwa katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI), Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo, Bw. Mvungi amepata fursa ya kujionea utekelezaji wa miradi hiyo, maendeleo yaliyofikiwa pamoja na mchango wake katika kuboresha mazingira ya utoaji wa mafunzo na kuongeza ufanisi wa Chuo cha Viwanda vya Misitu.

Ziara hiyo imelenga pia kufuatilia maendeleo ya miradi, kutathmini utekelezaji wake na kuhakikisha kuwa uwekezaji unaofanywa unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa maendeleo ya chuo na sekta ya misitu nchini.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi, ubora na kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.

13/08/2026

DIRISHA LA UDAHILI LIPO WAZI – CHUO CHA VIWANDA VYA MISITU (FITI)

Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kinapenda kuutaarifu umma kuwa dirisha la udahili kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada (Diploma) ya Teknolojia ya Viwanda vya Misitu limefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 28 Mei hadi 10 Julai 2026.

Sifa za Mwombaji

Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na kuwa na angalau ufaulu wa alama D nne (4), ambapo mbili (2) kati ya hizo ziwe za masomo ya sayansi. Wanafunzi wanapata mafunzo kwa vitendo kupitia mitambo, maabara na karakana za kisasa.

Kumbuka kuwa wanafunzi wa chuo chetu wanapatiwa mikopo na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Hivyo basi, unapofanya maombi ya kujiunga na chuo, kumbuka pia kuomba mkopo kupitia HESLB.

Karibu FITI upate taaluma na ujuzi wa uhifadhi wa misitu na matumizi endelevu ya mazao ya misitu.

Huduma za Hosteli

Hosteli zipo za kutosha kwa wanafunzi.

Mawasiliano

+255 786 704 784 – Afisa Udahili

+255 757 182 141 – Msajili wa Wanafunzi

+255 627 906 206 – Afisa Masoko

Barua Pepe

[email protected]

[email protected]

Heri ya Siku ya Wakulima .
08/08/2026

Heri ya Siku ya Wakulima .

Picha Mbalimbali za Wananchi waliojitokeza katika Banda la Chuo Cha Viwanda vya Misitu viwanja vya nzuguni jijini Dodoma...
07/08/2026

Picha Mbalimbali za Wananchi waliojitokeza katika Banda la Chuo Cha Viwanda vya Misitu viwanja vya nzuguni jijini Dodoma .

Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Edward Kohi leo Tarehe 7 Agosti 2026 ametembelea Band...
07/08/2026

Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Edward Kohi leo Tarehe 7 Agosti 2026 ametembelea Banda la Chuo Cha Viwanda vya Misitu lililopo katika Maonesho ya kimataifa ya Kilimo Nanenane viwanja vya nzuguni Jijini Dodoma.

DC NYANGASA AVUTIWA NA BIDHAA BUNIFU ZA FITI KATIKA MAONESHO YA NANENANEMkuu wa Wilaya ya Kondoa, Mheshimiwa Fatma Almas...
07/08/2026

DC NYANGASA AVUTIWA NA BIDHAA BUNIFU ZA FITI KATIKA MAONESHO YA NANENANE

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Mheshimiwa Fatma Almas Nyangasa, amevutiwa na bidhaa bunifu zinazotokana na mazao ya misitu zinazozalishwa na Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) baada ya kutembelea banda la chuo hicho katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Mheshimiwa Nyangasa alifanya ziara hiyo leo, tarehe 7 Agosti 2026, ambapo alipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kutokana na mazao ya misitu pamoja na teknolojia zinazotumiwa na chuo katika kuongeza thamani ya rasilimali za misitu.

Akiwa katika banda la FITI, Mkuu huyo wa Wilaya alipokea maelezo kutoka kwa waoneshaji wa chuo kuhusu mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya misitu, kuanzia uzalishaji wa malighafi, uchakataji, ubunifu wa bidhaa hadi matumizi yake. Pia alielimishwa kuhusu majukumu ya FITI katika kutoa mafunzo ya kitaaluma, kufanya tafiti na kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.

Mheshimiwa Nyangasa amesifu ubunifu unaofanywa na FITI, akieleza kuwa bidhaa hizo zina mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu, kuhamasisha ujasiriamali na kuchochea maendeleo ya uchumi kupitia sekta ya misitu.

Chuo Cha FITI kinaendelea kutumia Maonesho ya Nanenane k**a jukwaa la kuonesha teknolojia, bidhaa bunifu na fursa mbalimbali zinazopatikana chuoni, huku ikiendelea kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.

Address

Forest Industries Training Institute, Box 1925
Moshi

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255787676981

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Forest Industries Training Institute - FITI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Forest Industries Training Institute - FITI:

Shortcuts

Share

Category